Wakazi wa Bondo wakesha wakisubiri matokeo ya urais

Wakazi wa Bondo wakesha wakisubiri matokeo ya urais

NA WINNIE ONYANDO

WAKAZI wa Bondo Kaunti ya Siaya jana Jumatano walikesha nje ya Chuo Kikuu Cha Jaramogi Oginga Odinga (JOOUST) wakisubiri matokeo ya wanasasiasa mbalimbali ikiwemo ya mwaniaji urais Raila Odinga.

Wakazi hao walisema kuwa hawatalala hadi Bw Odinga atakapotangazwa mshindi.Wakiongozwa na Vincent Matara, mkazi wa Nyamira, karibu na boma la Jaramogi, alisema amesubiri ushindi wa Bw Odinga kwa muda na atakesha hadi atakaposikia kinara huyo wa ODM ametangazwa kuwa mshindi.

“Kama wakazi wa Bondo, tunatarajia ushindi wa Bw Odinga ambaye ni mmoja wetu,” akasema Bw Matara.

Kadhalika, Bw Matara alisema kuwa ushindi wa kiongozi huyo utakuwa mwamko mpya kisiasa kwa wakazi wa Bondo.

“Hii ni mara ya tano kiongozi huyo akisaka ushindi. Tuna imani kuwa atatangazwa mshindi,” akasema Bw Matara.

Tangu wakazi wapige kura, baadhi ya wanabishara wamefunga biashara zao wakisubiri ushindi wa Bw Odinga.

Kwingineko, watu zaidi ya wawili walijeruhiwa katika kituo cha kupiga kura cha Uyawi Dispensary baada ya wafuasi wa mwaniaji mmoja wa kiti Cha Udiwani Sakwa Kati, Bondo kuzua vurugu.

Kisa hicho kilifanya shughuli za kupiga kura kusimamishwa kwa muda.Wawili walidungwa kisu na gari la mwaniaji huyo kurushiwa mawe.

Maafisa wa polisi walifika katika eneo hilo na kutatua vurugu.

  • Tags

You can share this post!

Timo Werner arejea kambini mwa RB Leipzig baada ya kuagana...

NDIVYO SIVYO: Dhana ‘iko’ kwa maana ya ‘una’, mna,...

T L