Wakazi wa kaunti 22 wahitaji chakula cha msaada wa dharura

Wakazi wa kaunti 22 wahitaji chakula cha msaada wa dharura

NA JACOB WALTER

SHIRIKA la Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa huenda wakazi wa maeneo ya Kaskazini mwa Kenya wakaathiriwa zaidi na janga la njaa kufuatia uhaba wa mvua ulioshuhudiwa katika maeneo hayo.

Akizungumza Jumatatu wakati wa kugawa chakula cha msaada kwa watu walioathiriwa na njaa Kaunti ya Marsabit, afisa anayesimamia masuala ya ukaguzi na utekelezaji katika shirika la WFP, Samuel Kiarie, alisema wengi wataathiriwa zaidi ikiwa hatua mwafaka hazitachukuliwa.

“Maeneo ya Kaskazini mwa Kenya yamekosa mvua kwa muda mrefu. Hali hiyo imewaathiri wakulima na kufanya mazao kupungua. Hii ndio maana shirika la WFP limeamua kutoa msaada wa chakula kwa walioathiriwa,” akasema Bw Kiarie.

Alisema kuwa kaunti nane ziko hatarini kufuatia uhaba wa mvua.

Alieleza kuwa kaunti za Lamu, Kilifi, Taita Taveta, Tana River, Turkana, Samburu, Pokot Magharibi, Baringo, Kajiado, Narok, Laikipia, Nyeri, Embu, Meru, Tharaka Nithi, Makueni, Kitui, Marsabit, Isiolo, Wajir, Garissa na Mandera pia zimeanza kuathiriwa na uhaba wa chakula na hali hiyo itaendelea ikiwa serikali haitachukua hatua.

WFP ilisema inahitaji angalau Sh13 bilioni ili kupambana na janga hilo .

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Ni mwalimu mkuu na mwandishi stadi

Arsenal wapata kipa mpya kutoka Amerika

T L