Wakazi wa Kiambu wahimizwa wakumbatie kilimo

Wakazi wa Kiambu wahimizwa wakumbatie kilimo

NA LAWRENCE ONGARO

MBUNGE wa Thika Bw Patrick ‘Wajungle’ Wainaina, amesema Kiambu ina maeneo makubwa ya ustawishaji kilimo (High value Agriculture), ambayo yakitumiwa kwa njia ifaayo bila shaka kaunti hiyo itaongoza kwa kutoa mazao mengi.

Mbunge huyo alisema hata ingawa pia wakulima hupanda mahindi, maharage, na viazi, lakini wanastahili kuzingatia kilimo cha mazao mengine muhimu.

Alisema iwapo wakulima wangetaka kupata pesa ya kujikimu kimaisha wanastahili kupanda mazao aina ya macadamia, Avocado, na kuingilia pia ufugaji.

“Hata ingawa majanichai na kahawa imenawiri katika miaka za hapo awali lakini pia ni vyema kubadilisha mawazo kuhusu kilimo,” alifafanua Bw ‘Wajungle’

Bw ‘Wajungle’ aliyasema hayo Ijumaa alipozuru Thika Mashariki akiwahamasisha wakazi wa eneo hilo umuhimu wa kubadilisha mtazamo wao kuhusu kilimo.

Mbunge huyo pia anawania kiti cha ugavana Kiambu akimenyana na wawaniaji wengine watano.

Wiki moja iliyopita Bw Wajungle alizuru Gatundu na kusambaza miche ya macadamia na parachichi kwa zaidi ya wakazi wapatao 1,000.

Ametoa ahadi kwa wakazi wa Kiambu kwa ujumla ya kwamba iwapo atakuwa gavana wao, atazingatia maswala ya kilimo ili wakazi hao wawe na fedha za kujikimu na familia zao.

” Mimi natilia mkazo wakazi wa Kiambu wapande macadamia na parachichi kwa sababu ninajua mazao hayo ni kama dhahabu. Niko tayari kuwatafutia soko wakati wowote,” alisema Bw ‘Wajungle’.

Alisema iwapo kilimo kitatiliwa maanani ipasavyo bila shaka wakazi wa Kiambu hawawezi kukumbwa na janga la njaa.

  • Tags

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Muthoni ana siri kubwa ya darasa

Omurwa ajiunga na Sektzia Ness Ziona FC ya Israel

T L