Habari Mseto

Wakazi wa mitaa ya mabanda Nairobi wanakabiliwa na maradhi ya kupumua

October 23rd, 2019 1 min read

Na SAMMY KIMATU

WAKAZI katika mitaa ya mabanda ya Mukuru, Landi Mawe, Kaunti ya Nairobi, wameathiriwa pakubwa na maradhi ya kupumua.

Dkt Stewart Christina kutoka Shirika la Impactnations Amerika alisema hayo Jumatano kambi ya siku mbili ya matibabu bila malipo ilipokamilika katika Kanisa la Jeshi la Wokovu la Kayaba.

Kulingana na Dkt Mike Brawan, ambaye alihusika pia na kambi hiyo, watu zaidi ya 1,000 walipokea matibabu.

“Hii ni kambi ya mwisho baada ya Nakuru, Mombasa, Nakuru, Kisumu na Mogotio lakini baada ya kila miezi mitatu tutakuwa hapa,” Dkt Brawan alisema.

Aliongeza kuwa wataendelea na kambi zao kwa magereza na shuleni.