Wakazi waalikwa kwa hafla ya ‘kihistoria’ ya kuapisha Achani

Wakazi waalikwa kwa hafla ya ‘kihistoria’ ya kuapisha Achani

NA KNA

WAKAZI wa Kaunti ya Kwale, wameombwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia kuapishwa kwa gavana wa kwanza wa kike wa kaunti kuwahi kuchaguliwa ukanda wa Pwani.

Kaimu Katibu wa Kaunti ya Kwale, Bi Sylvia Chidodo, amesema maandalizi yamekamilika kumwapisha Bi Fatuma Achani kesho Alhamisi.

Hafla ya kuapishwa kwa Bi Achani na naibu wake, Bw Josphat Kombo Chirema, ambao walishinda kiti hicho kupitia Chama cha UDA, imepangiwa kufanyika katika uwanja mkuu wa Kwale kuanzia saa nne asubuhi.

Bi Achani, anayechukua mahali pa gavana anayeondoka, Bw Salim Mvurya, alisema hakuna muda wowote wa kupoteza kwa hivyo ataanza kazi mara moja atakapoapishwa ili kufanikisha ahadi alizotolea wananchi wakati wa kampeni.

Hata hivyo, wapinzani wake wamepanga kupinga ushindi wake mahakamani.

You can share this post!

Mbunge ataka korti izuiwe kumtuza Raila

Mungatana aapa kupigania haki za kaunti yake

T L