Habari za Kaunti

Wakazi wadai mrabaha kabla Base Titanium ifunganye virago

April 24th, 2024 1 min read

WAKAZI wa Kwale waliohamishwa ili kutoa nafasi kwa uchimbaji madini, wameitaka serikali kuharakisha kuweka mfumo utakaotumiwa kusimamia asilimia 10 ya ruzuku ya madini.

Haya yanajiri wakati kampuni ya Base Titanium ikitarajiwa kutamatisha uchimbaji madini.

Kampuni hiyo imekuwa ikiwasilisha malipo mbalimbali kwa serikali ikiwemo mrabaha ambao sehemu yake inafaa kuendea jamii.

Kulingana na sheria, jamii zinazoishi maeneo ambayo madini yanapatikana na yanachimbwa yanahitaji kupokea mirahaba ambayo kapuni za uchimbaji hulipa kwa serikali.

“Tumeahidiwa kulipa mrabaha kwa muda mrefu bila mafanikio. Uchimbaji madini sasa umefikia kikomo na hatujui kama bado tutafaidika,” Sabina Saiti, mkazi mmoja alisema.

Mratibu wa Muungano wa Kwale Mining Alliance, Kashi Jermaine, alitaka wakazi wawe na subira huku mikakati ikiwekwa jinsi ya kugawa pesa hizo.