Wakazi wafurahia minofu ya bure lori kukanyaga kondoo 48

Wakazi wafurahia minofu ya bure lori kukanyaga kondoo 48

Na Charles Wanyoro

Wakazi wa eneo la Makutano, Embu jana walifurahia mlo wa bure baada ya lori lililokuwa likiendeshwa kwa kasi kukanyaga mbuzi na kondoo 48 waliokuwa wakivuka barabara kando ya shule ya upili ya Wachoro barabara kuu ya Nyeri-Nairobi.

Mifugo hao walikuwa wakitoka malishoni wakati ajali hiyo ilitokea saa mbili usiku Jumatatu, wakiachwa aidha wakiwa wamekufa ama kujeruhiwa.

Wakazi wa kijiji cha Karuku na Makutano walikimbia eneo la ajali, wakawalemea wachungaji waliokuwa wakichunga na kuondoka na minofu na mizoga.

Kufuatia kisa hicho, hali ya usafiri katika barabara hiyo iliathiriwa kwa muda hadi wakazi walipomaliza kukusanya mifugo hao.

 

You can share this post!

Yaibuka aliyeuawa aliiba mbuzi wa mwalimu wake

UTAMADUNI: Ngombe 14 wanatosha kufidia kifo cha mwana...

adminleo