Habari Mseto

Wakazi wakerwa hafla ya msaada ilipogeuzwa kuwa mkutano wa hadhara

April 12th, 2024 1 min read

Na SAMMY KIMATU

WAATHIRIWA wa mafuriko kutoka mitaa kadhaa ya Mukuru katika tarafa ya South B, Nairobi walipandwa na hasira, baada ya hafla waliyoalikwa jana asubuhi kuwapa misaada kugeuzwa mkutano wa hadhara.

“Tuliambiwa tukusanyike katika eneo la Kartasi mkabala wa barabara ya Entreprise kabla ya saa mbili na nusu asubuhi. Pia tulihitajika kuwasilisha majina yetu na simu zetu kwa kiongozi wa timu yetu kabla ya kuanza kwa hafla hiyo,” alisema Bw Christopher Madevu Lunalo.

Naibu Kamishna wa Kaunti ya Starehe, Bw John Kisang, alifafanua kuwa mkutano huo ulihusu hatua zitakazochukuliwa na serikali katika kushughulikia suala la kudumu la kukabili athari za mafuriko na unyakuzi wa ardhi katika kingo za mto Ngong na barabara ya Enterprise.