Wakazi watakiwa kuunga mkono serikali ya Ruto

Wakazi watakiwa kuunga mkono serikali ya Ruto

NA WINNIE ATIENO

VIONGOZI wa kisiasa wanawake kutoka kaunti ya Taita Taveta wamewataka wakazi kuunga mkono serikali kuu inayoongozwa na Rais William Ruto ili kufaidi kwa maendeleo.

Wanawake walisema ushirikiano na serikali kuu itafaidi kaunti hiyo hasa kwa maendeleo.

“Tusiposhirikiana na serikali kuu ili tupate maendeleo tutasalia nyuma,” alisema Annah Nyambu.

Mwenyekiti kikundi cha Taita Taveta Women for Change, Bi Racheal Mwakazi alisema ataendelea kuhamasisha wakazi kuhusu siasa.

“Ni muhimu kuchagua wanawake kwenye siasa,” alisema Bi Mwakazi.

Walisema wataendelea kuchunga kaunti hiyo ili wananchi wafaidike kwa maendeleo.

Walisema kaunti hiyo inafaa inufaike na madini na raslimali zilizosheheni kaunti hiyo.

  • Tags

You can share this post!

DARUBINI YA WIKI: TOLEO NAMBARI 4, Septemba 25, 2022

Wanaharakati wataka usalama uimarishwe Malindi

T L