Wakenya kuanza kula mahindi yaliyokuzwa kutumia mbinu ya GMO

Wakenya kuanza kula mahindi yaliyokuzwa kutumia mbinu ya GMO

NA PSCU

SERIKALI imeondoa marufuku ya uzalishaji na uagizaji wa vyakula vilivyokuzwa kisayansi, maarufu GMO, kama hatua za dharura za kuokoa maelfu ya Wakenya wanaokumbwa na njaa.

Kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri chini ya uwenyekiti wa Rais William Ruto jana Jumatatu, iliamualiwa serikali ianze kutekeleza mapendekezo ya jopokazi lililochunguza kuhusu vyakula vya GMO na usalama wake kwa binadamu.

Taarifa kutoka Ikulu ya Nairobi ilisema hatua hiyo inalenga kuokoa maisha ya watu na mifugo katika kaunti 23 zinazoathiriwa na kiangazi.

“Baraza la Mawaziri limefuta uamuzi wa Novemba 8, 2012 ambao ulipiga marufuku ukuzaji na uagizaji wa vyakula vya binadamu na lishe ya mifugo iliyoundwa kiteknolojia. Kwa uamuzi huu, sasa inaruhusiwa kukuza au kuagiza kutoka nje vyakula vya GMO,” ikasema taarifa hiyo.

Baraza la Mawaziri pia lilijadili na kuzingatia mapendekezo kadhaa yanayohusiana na mbinu za kukabili mabadiliko ya mazingira, kupunguza kilimo kinachotegemea mvua, kukuza mazao yanayohimili kiangazi na utekelezaji wa hatua za kutoa onyo la mapema kuhusu maafa.

Wiki jana, serikali ilizindua msaada wa chakula kwa kaunti 23 za maeneo kame nchini na inapanga kushirikiana na kiwanda cha nyama (KMC) ili kununua mifugo kutoka kwa wafugaji walioathiriwa.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamke aondoa kesi dhidi ya Linturi

Wafanyibiashara walia kukosa biashara kituo cha mizigo cha...

T L