Wakenya kupokea kwa hiari chanjo ya Covid-19

Wakenya kupokea kwa hiari chanjo ya Covid-19

Na SAMMY WAWERU

CHANJO kuzuia kuambukizwa virusi hatari vya corona itatolewa kwa watakaohiari kuipokea, imesema serikali ya Kenya.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema hakuna atakayeshurutishwa kuchanjwa, chanjo inayotarajiwa nchini itakapowasili.

“Itakopofika tuanze kusambaza hakuna atakayelazimishwa kuchanjwa, watu watachanjwa kwa hiari,” akasema Bw Kagwe.

Alisema hayo Ijumaa kwenye kikao na wanahabari katika makao makuu ya idara ya afya, Nairobi.

Waziri Kagwe hata hivyo hakueleza iwapo chanjo ya Covid-19 itatozwa malipo.

Uingereza ndiyo ilikuwa ya kwanza kabisa kuanza kuwapa raia wake chanjo ya Covid-19 ambayo kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonyesha inazuia binadamu kuambukizwa.

Bw Kagwe aliambia waandishi wa habari kwamba Kenya haitategemea chanjo ya taifa moja pekee.

“Tunatafuta chanjo ya mataifa mengine iliyoidhinishwa. Hatutategemea nchi moja pekee,” akaelezea.

You can share this post!

Shule zinapofunguliwa tuwe waangalifu Covid-19 isitulemee...

Watford wajinasia fowadi matata kutoka Ligi Kuu ya Norway