Wakenya kushiriki Jumuiya ya Madola ya chipukizi Trinidad & Tobago

Wakenya kushiriki Jumuiya ya Madola ya chipukizi Trinidad & Tobago

Na GEOFFREY ANENE

KENYA itashiriki uogeleaji, riadha, uendeshaji wa baiskeli, triathlon, raga ya wachezaji saba kila upande na voliboli ya ufukweni kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya chipukizi nchini Trinidad & Tobago mnamo Agosti 4-11.

Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) imesema kuwa wasichana kutoka Kenya watawania ubingwa katika fani hizo zote sita nao wavulana katika uogeleaji, riadha, uendeshaji na triathlon.

Kenya itakosa fani moja pekee – mpira wa pete wa aina ya Fast5 ambao ni mfupi na unachezwa kwa kasi ya juu.

Ikiadhimisha siku ya Jumuiya ya Madola hapo Machi 13, NOC-K pia ilisema kuwa imechagua wachezaji wanne chipukizi walemavu kupokea udhamini wa kimichezo kupitia mradi wa vijana wa GAPS.

Usaidizi huo wa kifedha utafanikisha mazoezi yao na kufuzu kwa michezo hiyo ya Jumuiya ya Madola.

Wachezaji hao ni Cynthia Muthoni, Beryl Achieng, Titus Mwonga Maundu na Nicholas Kalonzo. Watakuwa chini ya makocha Merab Imai, Edmon Bett, Michael Omondi na Rose Inaruhiu. 

  • Tags

You can share this post!

Chuo chatimua wanafunzi wenye vyeti feki vya KCSE

ZARAA: Hawasubiri misaada tu, wao wanajikuzia chakula

T L