Wakenya waendea medali za dhahabu ndondi za Ukanda wa Tatu jijini Kinshasa

Wakenya waendea medali za dhahabu ndondi za Ukanda wa Tatu jijini Kinshasa

Na GEOFFREY ANENE

MASHINDANO ya masumbwi ya Afrika ya ukanda wa tatu yatafikia kilele mjini Kinshasa hii leo Ijumaa, ambapo Wakenya watano wanawinda dhahabu.

Christine Ongare (uzani wa kilo 51), Nick ‘Commander’ Okoth (kilo 57) na Elly Ajowi (zaidi ya kilo 91), ambao wamefuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki baadaye mwaka huu, wako katika fainali ya vitengo hivyo vyao.

Ongare atalimana na Munga Zalia (DR Congo) katika pigano ambalo Mkenya huyo atalenga kulipiza kisasi baada ya kuona vimulimuli walipokutana hapo mapema katika mashindano haya yaliyovutia mataifa saba.

Commander hajapoteza pigano lolote. Atapimwa vilivyo ubora wake dhidi ya raia wa Cameroon Tchouta Mbianda Ignas Aristide Ron. Ajowi pia atakuwa kwenye mizani ya Mkameruni Maxime Yegnong Njieyo.

Wakenya wengine katika fainali ni David Karanja dhidi ya Muntu Biakulolowa (DR Congo) katika uzani wa kilo 52, naye Boniface Mugunde atachapana na Kayla (DR Congo) katika uzani wa kilo 69.

Hapo Jumatano, Mkenya mwingine anayeenda Olimpiki, Elizabeth Akinyi, alizidiwa nguvu na Mbabi (DR Congo) katika uzani wa kilo 69.

  • Tags

You can share this post!

Wanasiasa wa Mlima Kenya walia ‘kunyanyaswa’ na rais

Covid: Wanaohepa chanjo kuadhibiwa