Michezo

Wakenya watwaa dhahabu Mbio za Nyika Algeria

March 18th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

WAKENYA Celliphine Chespol, Ronex Kipruto na Alfred Barkach wamezoa medali za dhahabu katika Mbio za Nyika za Afrika mjini Chlef nchini Algeria, Jumamosi.

Chespol na Barkach wametwaa ushindi katika mbio za watu wazima zilizojumuisha kilomita 10. Kipruto amevuna dhahabu katika mbio za wanaume wasiozidi umri wa miaka 20 zilijumuisha kilomita nane.

Margaret Chelimo alimaliza na medali ya fedha katika mbio za kilomita 10 za wanawake naye Stanley Waithaka akajishindia medali hiyo katika mbio za wanaume za kilomita nane.

Kenya pia ilishinda medali ya fedha katika mbio za kilomita 10 za wanaume kupitia Julius Kogo naye Helen Ekalale akanyakua nishani ya shaba katika mbio za kilomita sita (wanawake wasiozidi umri wa miaka 20).

Mirriam Cherop, ambaye alikuwa akitetea taji la wanawake la Under-20, alimaliza katika nafasi ya sita.

Katika mbio za kilomita nane za mseto, Ethiopia iliibuka mshindi kwa dakika 23:52. Ilifuatwa kwa karibu na Kenya (24:15) nazo Morocco na Algeria zikamaliza katika nafasi za tatu na nne kwa dakika 25:07 na 25:51, mtawalia.

Matokeo ya 10-bora (Machi 17, 2018):

Wanawake (kilomita 10)

Celliphine Chespol (Kenya) dakika 35:10

Margaret Chelimo (Kenya) 35:13

Yeshi Kalayu (Ethiopia) 35:26

Stacy Ndiwa (Kenya) 35:27

Stella Chesang (Uganda) 35:30

Sandra Chebet (Kenya) 35:47

Mercyline Chelangat (Uganda) 35:53

Rosemary Njeri (Kenya) 36:01

Gate Mayehu (Ethiopia) 36:08

Wanaume (kilomita 10)

Alfred Barkach (Kenya) dakika 30:47

Julius Kogo (Kenya) 30:47

Thomas Ayeko (Uganda) 30:47

Enyew Mekonnen (Ethiopia) 31:01

Emmanuel Bor (Kenya) 31:14

Philip Kipyeko (Uganda) 31:19

John Chepkwony (Kenya) 31:22

Filmon Ande (Eritrea) 31:23

Mande Bushendich (Uganda) 31:26

Tesfaye Berhe (Ethiopia) 31:28

Wanawake U/20 (kilomita sita)

Egziabher Gebru (Ethiopia) dakika 20:40

Selama Gebrerufal (Ethiopia) 20:54

Hellen Ekalale (Kenya) 20:55

Agnes Jebet (Kenya) 21:02

Roselidah Jepketer (Kenya) 21:04

Mirriam Cherop (Kenya) 21:06

Mizan Alem (Ethiopia) 21:08

Edinah Jebitok (Kenya) 21:21

Ejgayehu Taye (Ethiopia) 21:23

Beatrice Chebet (Kenya) 21:32

Wanaume U/20 (kilomita nane)

Ronex Kipruto (Kenya) dakika 25:01

Stanley Waithaka (Kenya) 25:06

Solomon Berihu (Ethiopia) 25:08

Berehanu Wendim (Ethiopia) 25:11

Milkesa Mengesha (Ethiopia) 25:13

Vincent Kipkemoi (Kenya) 25:14

Edwin Kiplagat (Kenya) 25:17

Edward Zakayo (Kenya) 25:20

Dominic Kiptum (Kenya) 25:31

Nibret Melak (Ethiopia) 25:34