Habari Mseto

Wakili Gicheru kizimbani ICC leo Ijumaa

November 6th, 2020 1 min read

Na VALENTINE OBARA

WAKILI Paul Gicheru, anayedaiwa kushawishi mashahidi wajiondoe katika kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 iliyomkumba Naibu Rais William Ruto, anatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) leo Ijumaa.

Bw Gicheru, ambaye alijisalimisha kwa polisi wa Uholanzi mnamo Jumatatu, alipelekwa seli Jumanne.

Amepangiwa kuwasilishwa mbele ya Jaji Reine Adélaïde Sophie Alapini-Gansou anayetarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu kesi hiyo.