Habari Mseto

Wakili mashakani kwa kupokea mamilioni kilaghai

August 25th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

WAKILI mmoja alishtakiwa Ijumaa kwa kupokea Sh3.7 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Bw Anambo Alex alikana kupokea pesa hizo kutoka kwa Bw Humphrey Mwenda Mung’ori akidai angemuuzia shamba jijini Nairobi.

Alishtakiwa alisemekana alikuwa amemweleza Bw Mung’ori atamuuzia shamba lenye ukubwa wa ekari 0.0202.

Shtaka lilisema alijaribu kupokea pesa hizo kati ya  Julai 11, 2017 na Mei 15 mwaka huu.

Wakili alikabiliwa na shtaka la pili ya kujaribu kumlaghai tena Bw Mung’ori Sh5.5 milioni.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 pesa taslimu.