Wakili Yano asema atakuwa akiuliza kuhusu hisia za Rais

Wakili Yano asema atakuwa akiuliza kuhusu hisia za Rais

Na RICHARD MUNGUTI

MWANIAJI wa 10 anayewania wadhifa wa Jaji Mkuu Ijumaa alishangaza tume ya huduma za mahakama (JSC) aliposema atakuwa anampigia mke wa Rais Uhuru Kenyatta kujua hisia zake kabla ya kumpigia simu kujadili masuala nyeti ya idara ya mahakama kama uapishwaji wa majaji 41.

“Nitakuwa ninampigia simu mkewe Rais Bi Margaret Kenyatta kujua hisia za (Mzee) Rais Uhuru Kenyatta ndipo nimpigie simu kumueleza changamoto ninazokumbana nazo katika utekelezaji kazi yangu kama Jaji Mkuu,”  wakili  Bi Alice Jepkoech Yano alisema akijibu maswali.

Bi Yano, ambaye ni mwaniaji wa 10 kuhojiwa katika mchakato wa kumsaka mrithi wa Bw David Maraga alisema idara ya mahakama inakabiliwa na changa moto chungu nzima zinazohitaji kutatuliwa.

Alisema masuala kama vile ufisadi, kupotea kwa faili za kesi, mrundiko wa kesi ambao umefikia milioni moja ni miongoni mwa changamoto alizosema atazishughulikia endapo atateuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Akihojiwa na Kamishna Everlyne Olwande, Bi Yano alishindwa kueleza sababu kesi aliyoshtakiwa na mteja wake imekaa katika mahakama ya Eldoret miaka minane kabla ya kuamuliwa.

“Je ikiwa unataka kesi ziwe zikikamilishwa kwa muda mfupi mbona kesi uliyoshtakiwa na mteja wako imechukua muda wa miaka minane kuamuliwa. Je ukiteuliwa Jaji Mkuu kweli utakuwa na hari ya kuharakisha kesi,” Bi Olwande alimwuliza Bi Yano.

Akijibu alisema , “ Kesi yangu inaendelezwa na wakili niliyemteua na siwezi kuijadilia hapa.”

Bi Olwande alimweleza Bi Yano kuwa kuna kesi nyingine aliyoshtakiwa na hiyo amejibu katika mawasilisho yake kwa tume.

Alisema Jaji Mkuu wa 15 atakayeteuliwa kumrithi Jaji Maraga sharti akumbatie matumizi ya teknolojia katika ukamilishaji wa kesi kwa muda mfupi.

Pia alisema teknolojia itapunguza ufisadi kwa vile  mbali mbali zinazohitaji kusuluhishwa mara moja.

Mwaniaji huyo alisema ijapokuwa vitengo vyama mahakama vinaongozwa na wanawake “wakati ni sasa Jaji Mkuu kuwa mwanamke.”

Wakili huyo mwenye tajriba ya miaka 25 alikabiliwa na wakati mgumu kueleza majukumu ya kamati mbali mbali za idara ya mahakama.

Bi Yano alieleza JSC kwamba mumewe aliaga miaka miwili iliyo na kuachwa na watoto wawili anaoendelea kuwalea.

Alishindwa kabisa kufafanua sheria kuhusu sheria iliyopelekea kuharamishwa kwa adhabu ya kifo.

Pia alisema kuwa uaumuzi huo wa mahakama ya juu unakanganya na mahakimu wanautumia vibaya.

Mwenyekiti wa mchakato huo Prof Olive Mugedi alisitisha vikao vya mchakato huo hadi Mahakama iamue kuhusu uhalali wa harakati hizo.

  • Tags

You can share this post!

Polisi aliyeua Floyd hatarini kusukumwa jela miaka 40

Wanaodai Magufuli aliuawa kwa sumu wajitokeze – Rais...