Wakongwe wanavyoangamia wakimumunya raha ya dunia

Wakongwe wanavyoangamia wakimumunya raha ya dunia

NA WANGU KANURI

WAKENYA wanazidi kushangazwa na wazee waliokonga wanapozidi kuiaga dunia katika anasa za dunia, wakilemewa na kazi wanayoamini inawapa utulivu wa mwili na akili, na kuishisia kutumia vidonge vya kuongeza nguvu za kiume.

Kama tamu yaua sumu ya nini? Marehemu David Mluli, aliyekuwa na miaka 80, anaingia kwenye takwimu za hivi karibuni za watu waliofariki dunia wakimumunya uroka katika mzinga ya vidosho wa umri wa wajukuu wao.

Mluli alikuwa akimenya tunda la Neema Kibaya, king’asti mwenye umri wa miaka 33, kabla ya moyo wake kufeli na mwili wake kuzimia.

Kwenye uchunguzi wao, polisi nchini Tanzania wamethibitisha kuwa, hakukuwa na majeraha, ila chupi ya marehemu ilikuwa na matone ya manii kabla ya kuelekea njia ya marahaba.

Siku chache kabla ya tukio la Tanzania, nchini Kenya mzee mwenye umri wa miaka 60 katika Kaunti ya Mombasa alifia juu ya mapaja ya binti mmoja na kufikisha wanne, idadi ya wazee waliokufa kwa kuramba asali.

Stephen Kariuki, alilalamikia maumivu ya kifua wakati wa kushiriki ngono na Esther Karimi mwenye umri wa miaka 33 lakini akaaga punde tu baada ya kufikishwa katika hospitali ya Bomu, Changamwe.

Kisa hiki kinatokea siku kumi na moja baada ya mwanamume mwingine mwenye umri wa miaka 35, Dandora, Nairobi kuzirai na kuaga baada ya kushiriki katika tendo la ndoa.

Mwendazake Robert Maina, mwajiriwa wa hospitali ya Kenyatta alikuwa akirushana roho na mpenziwe Joyce Wairimu wakati ambapo alilemewa kumeza asali na kupumua pumzi ya mwisho.

Mwanzoni mwa Januari 2021, marehemu Kirimi Nkunja aliipungia dunia mkono wa buriani kwa tukio lililotatanisha. Hivi ni baada ya mwili wake kupatikana bila nguo kwenye chumba cha kulala mjini Maua, Igembe Kusini, Kaunti ya Meru.

Mwanamume huyu ambaye alifika katika chumba cha kulala cha New Ben Bella akiandamwa na wanawake wawili, alipatikana na wafanyikazi hotelini hiyo huku wanawake hao wawili wakiwa hawapo kwenye chumba hicho wakati ambapo mwili ulipatikana.

Visa hivi vinaibua hisia na maswali chungu nzima huku wengi wakiuliza kwa nini wanaume wanakunywa dawa hizi za kuongeza nguvu wanaposhiriki ngono.

Isitoshe, je tendo hili la ndoa linafikia wapi linakuwa karaha? Je, ni lazima mwanamume ale uroda na ayahatarishe maisha yake? Maswali haya yaliibua gumzo katika mitandao ya kijamii, huku wakenya wakiwa na haya ya kusema:

“Wanaume tuwache viagra, ni nini kilifanyika kwa chuma ya Doshi?” akauliza @Andrewodera6. “Inastaajabisha vile daima ni mwanamume hufa,” akasema @Paulondeng.

“Serikali lazima ipige marufuku kidonge aina ya viagra haraka. Ikiwa kidonge hiki hakitapigwa marukufu hivi karibuni kitawamaliza wanaume wetu,” akaandika @speakkam.

“Wanaume tutamalizika na hivi vitu ghushi,” akasema @MGithuga. “Afya ya ‘wanajeshi’ hawa inapaswa kuangaziwa mara kwa mara haswa kabla hawajatumwa kwa misheni,” akaandika Steven Winword.

“Ninafikiri kuwa vyumba hivi vya kulala na hoteli vinapaswa kuwapatia wanaume wazee vyakula spesheli kwanza na tena wahakikishe kuwa wamewaajiri madaktari waliobobea kwenye kazi ili waangalie afya za wateja wao pindi tu wamejihifadhia chumba,” akasema Monica Mailo.

 

“Wanaume wazee hawana adabu ambao hawana heshima za familia zao. Mungu awasamehe,” akawashutumu Jane Kamau.

“Tamaa hapo ndipo humfikisha mtu… angeridhika na kile alikuwa anapata kutoka kwa mkewe,” akasema Faith Amoure.

Bila kusahau kuwa tendo la ndoa kwa wanandoa ni kigezo muhimu cha ndoa, ukahaba na matumizi ya dawa kwa minajili ya kushiriki ngono ni baadhi ya mambo ambayo yanawaua wanaume.

Kula uroda ni sababu kuu ya kudorora kwa adabu kati ya wanandoa huku mmoja wao akitafuta njia mbadala ya kukata kiu yake.

Isitoshe, uhusiano wa wasichana wapevu na wanaume wazee umechangia vifo hivi huku ikiwalazimu wanaume husika kunywa dawa hizi za kuongeza nguvu wakati wa tendo hilo.

Kwa mujibu wa Zara Risoldi Cochrane, amabye ni mwanafamasia, matumizi ya dawa hizi bila kipimo unachangia pia ongezeko la vifo vya wanaume kwani nyongeza ya dawa hizi hufanya mwili kufanya kazi zaidi ya kawaida.

“Hii ina maana kuwa uchu wa mwanamume unafanyishwa kazi kupita kiwango kinachofaa huku ukichosha viungo vingine vya mwili. Kwa mfano ujapokunywa Viagra kupita kiwango kinachofaa, uchu wa mwanamume hubaki umesisimka kwa saa nusura nne huku tishu za uchu wake zikiharibiwa. Hii ni kwa sababu, damu iliyoko kwenye uchu wake haipokei okisijeni yoyote,” akaeleza Taifa Leo Dijitali.

You can share this post!

Kwa kila tone la mvua, wakazi wahofia usalama wao

Wanajeshi wa Uganda wamzima balozi wa Amerika kumtembelea...