Wakufunzi zaidi ya 400 wameshtaki vyuo vikuu viwili kwa nyongeza ya mishahara

Wakufunzi zaidi ya 400 wameshtaki vyuo vikuu viwili kwa nyongeza ya mishahara

Na RICHARD MUNGUTI

WAKUFUNZI zaidi ya 400 wameshtaki vyuo vikuu viwili vya umma wakiomba nyongeza ya mishahara ya zaidi ya Sh200milioni.

Katika kesi mbili zilizoshtakiwa na chama kutetea wafanyakazi katika vyuo vikuu (Uasu) wakufunzi hao wanadai haki zao zimekandamizwa na waajiri wao. Uasu kimeshtaki vyuo vya Maasai Mara University (MMU) na Chuo kikuu cha Kiufundi Nchini (TUK).

Chama hiki kinaomba mahakama ya kuamua mizozo ya wafanyakazi (ELRC) iamuru vyuo hivyo vilipe wakufunzi. Wakufunzi hao wanasema pesa hizo ni malimbikizi ya mishara yao ya muda wa miaka tisa kati ya 2013 na 2021. Wakufunzi hao 421 wameeleza mahakama haki zao za kupokea mishahara iliyopitishwa katika makubaliano na baraza la kuajiri wahudumu katika vyuo vikuu (IPUCCF) zimekandamizwa.

Jaji Maureen Odero aliyesikiza kesi hizo aliziratibisha kuwa za dharura na kumwagiza wakili Titus Koceyo akabidhi vyuo hivyo nakala za mashtaka katika muda wa siku saba. Bw Koceyo alimsihi Jaji Onyango atumie mamlaka na uwezo aliopewa na sheria kushurutisha MMU na TUK zitoe malipo hayo.

Katika kesi ya chuo cha MMU Jaji Onyango alielezwa na Koceyo kwamba kimekataa kuwalipa wakufunzi 176 mishahara iliyokubalianwa wakati wa mkataba wa mwaka wa 2017-2021 wa miaka minne. Badala yake MMU kimekoma kulipa kwa mujibu wa mkataba (CBA) huo wa 2017-2021 na kurejelea kutumia mkataba wa 2013-2017 ambao umepitwa na wakati.

Uasu kinaomba TUK ikilipe zaidi Sh108milioni ambazo ni ada ilizowakata wakufunzi na kukataa kusalamisha kati ya 2015 na 2021.

You can share this post!

Wazalendo: Tulipata mafunzo kwa kupigwa kwa hivyo...

Nyumba ya gaidi wa Al Shabaab kutwaliwa na serikali

T L