Habari Mseto

Wakurugenzi wa benki wataka viwango vya riba vidhibitiwe

June 25th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Wakurugenzi katika sekta ya benki wanaunga mkono kudhibitiwa kwa viwango vya riba.

Hii ni licha ya kusukuma kubadilishwa kwa Sheria ya Benki ili kuimarisha uwezo wa kupata huduma za benki.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Oxford Business Group (OBG), iliyojumuisha wakurugenzi wakuu 136.

Utafiti huo ulionyesha asilimia 89 ya wakurugenzi wanaunga mkono kudhibitiwa kwa viwango vya riba kwa mikopo, kwa kusema hatua hiyo ilikuwa imeimarisha gharama ya kupata mikopo.

Benki hata hivyo ziliacha kupea mikopo baadhi ya watu au mashirika zinazohisi ni hatari kwa biashara zao.

Kwa sasa viwango vya riba ni asilimia nne juu ya viwango vinavyotozwa benki na Benki Kuu ya Kenya.

“Ingawa mikopo inaonekana kuwa rahisi, imekuwa vigumu kuchukua mkopo nchini,” alisema Souhir Mzali, Mkurugenzi Mkuu wa OBG eneo la Afrika, na kuongeza kuwa biashara ndogo ndizo ziliathiriwa na hatua hiyo.