Wakurugenzi wa kampuni ya kuuza sukari wako na kesi ya kujibu

Wakurugenzi wa kampuni ya kuuza sukari wako na kesi ya kujibu

Na RICHARD MUNGUTI

WAKURUGENZI watatu wanaoshtakiwa katika kashfa ya sukari ya Sh79milioni wako na kesi ya kujibu.

Hakimu mkuu Bi Roseline Onganyo alisema kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Mabw Sunil Narshi Shah, Kamal Narshi Punja Shah na Magnesh Kumar Verma wa United Millers Limited (UML) kuwezesha mahakama iwaamuru wajitetee.

Wakurugenzi hao wanadaiwa walikula njama kulaghai kampuni ya B N Kotecha & Sons Limited Sh79, 471,000 wakidai alikataa kuwapelekea sukari. Ushahidi uliowasilisha kortini ulisema watatu hao pamoja na meneja wao wa mauzo Bw Munywoki Kavita walitumia nakala LPO za wamiliki wa biashara eneo la Mlima Kenya kudai malipo ya Sh79milioni kutoka kwa kampuni ya B N Kotecha & Sons.

Walitumia nakala hizi za LPO kushtaki B N Kotecha wakiomba mahakama kuu ya Kisumu iwamuru walipwe fidia ya Sh79milioni. Watatu hao walieleza mahakama kuu Kisumu walipata hasara kubwa B N Kotecha iliposhindwa kuuzia UML sukari kuwapelekea wafanya biashara hao wa eneo la Mlima Kenya miaka sita iliyopita.

Mahakama ilisema wakurugenzi hao watajitetea kwa mashtaka saba. Wataanza kujitetea mnamo Desemba 15,2021. Walikanusha mashtaka yote saba.

Hakimu mkuu Roseline Onganyo…Picha/RICHARD MUNGUTI

You can share this post!

300 wapewa vyeti vya uendeshaji boti

Matumaini Achani huenda akapeperusha UDA Kwale

F M