Habari Mseto

Wakwepaji ushuru kuzimwa na mfumo mpya wa dijitali

January 23rd, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Watu binafsi na kampuni zitakazokataa kutangaza ushuru wao watafungiwa nje katika biashara ya uagizaji na uuzaji nje ya nchi.

Tangazo hili lilitolewa na Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) kwa lengo la kuhakikisha wananchi wametangaza ushuru.

Kulingana na mamlaka hiyo, itakuwa rahisi kujua watu wanaodanganya kuhusu ushuru wao kupitia kwa mfumo mpya wa kielektroniki (iCMS) utakaounganishwa na mfumo wa kutangaza ushuru mtandaoni, iTax.

“Itakuwa rahisi kushirikisha habari katika iTax ili wanunuzi nje ambao hawajatangaza ushuru wa nyumbani wasiwe na uwezo wa kutangaza ushuru kutokana na mauzo ya nje,” alisema kamishan mkuu John Njiraini.

Kutokana na hilo, ni vigumu sana kwa mfanyibiashara kuagiza bidhaa kutoka nje.

Chama cha Watengenezaji Bidhaa (KAM) kilikaribisha hatua hiyo. Awali, chama hicho kilishutumu bandari ya Mombasa kwa kuwezesha ukwepaji wa ushuru kutokana na usafirishaji wa bidhaa kwa njia haramu.