Habari Mseto

Walaghai kuzimwa kupata msaada wa wanaoishi na ulemavu

April 23rd, 2024 1 min read

NA KNA

SERIKALI imeweka mipango maalumu ili walaghai wasinufaike na ufadhili unaotolewa kwa watu wanaoishi na ulemavu.

Naibu Kamishna wa eneo la Pwani, Mbogho Majioe, alisema kila mmoja aliyejiandikisha hufanyiwa utathmini wa kina, kisha hufuatiliwa ili kuthibitisha anavyotumia ufadhili aliopokea.

Alisema hayo wakati Hazina ya Kitaifa ya Walemavu nchini ilipokuwa ikiendeleza mpango wake wa kuwezesha watu wanaoishi na ulemavu, kwa kuwapa vifaa vya kuendeleza biashara na ufadhili wa elimu.