Walemavu wafurahia zawadi ya Krismasi

Walemavu wafurahia zawadi ya Krismasi

NA CHARLES ONGADI

MOMBASA

HUKU sherehe za Krismasi na mwaka mpya zikiwa pua na mdomo, walemavu 70 walipokea zawadi kutoka kwa msamaria mwema.

Ilikuwa ni zawadi ya vyakula kutoka kwa mkurugenzi wa Coast Legal Resource Foundation Bw Joseph Juma Mukewa iliyo na makao yake jijini Mombasa.

“Ni kipindi cha sherehe na mara nyingi walemavu husahaulika wkrismasakati huu na ndiposa mimi na familia yangu tumeamua kutoa kidogo tulichonacho kuwafaa wenzetu hawa, “ akasema Bw Mukewa wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi hizi katia ofisi za Coast Legal Resource Foundation eneo la Sabasaba, Mombasa.

Walemavu hao walitoka maeneo ya Likoni, Changamwe, Kisauni na Mvita na Jomvu walipokea unga tatu kila mmoja, mafuta ya kupikia, sukari na chumvi.

Mbali na vyakula hivyo, Bw Mukewa pia aliwagawanyia vitabu maalum vya Bibilia kwa wasioona ili waweze kusoma kipindi cha sherehe ya Krismasi.

Akizungumza na Taifa Leo online baada ya kupokea zawadi hizo Bw John Mkalla ambaye ni mlemavu asiyeona (Kipofu), alimshukuru Bw Mukewa za kuweza kuwafaa kipindi hiki cha sherehe.

“Baadhi yetu hatukujua tungesheherekea vipi sikukuu ya Krismasi kutokana na hali ilivyo kwa sasa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona lakini sasa tutaweza kula na kunywa kama tu wenzetu wengine, “ akasema kwa bashasha Bw Mkalla.

Bw Mukewa ambaye pia mwanachama wa bodi ya Shirika la Chhristian Human Rights For Justice amewataka walemavu kutonyamaza haki zao zinapokiukwa kipindi hiki cha sherehe.

“Ripotini visa vya dhuluma dhidi yenu katika ofisi zetu wakati wowote na hasa kipindi hiki cha sherehe za Krismasi na mwaka mpya ili kupata haki,” akawashauri Bw Mukewa.

Bw Mukewa amewaomba wahisani zaidi kujitokeza kuwafaa walemavu kwa hali na mali kiindi hiki cha sherehe za Krismasi na mwaka mpya.

You can share this post!

Siombi radhi, Wambua ni dume katili, Nzilani sasa asema

Hospitali ya Gatundu yapanda ngazi