Walimu 200,000 wapewa mafunzo ya kutekeleza CBC

Walimu 200,000 wapewa mafunzo ya kutekeleza CBC

NA JOSEPH OPENDA

WALIMU 200,000 wamepatiwa mafunzo kuhusu mtaala wa elimu wa Umilisi na Utendaji (CBC) katika maandalizi ya masomo ya Gredi ya Sita.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Huduma ya Walimu (TSC), Bi Nancy Macharia alisema Wizara ya Elimu inajitahidi kuhakikisha wanafunzi hawatatizika wakiingia gredi zijazo.

Kulingana na Bi Macharia, walimu zaidi watapatiwa mafunzo kuanzia Aprili.Kundi la kwanza la mtaala wa CBC, ambalo kwa wakati huu liko gredi ya tano linatarajiwa kujiunga na Gredi ya Sita Aprili 27 shule zitakapofunguliwa kwa mwaka mpya wa masomo.

Mkuu huyo wa TSC alisema hayo akiwa Nakuru kusimamia usambazaji wa karatasi za mtihani wa kidato cha nne (KSCE) ulioanza Jumatatu.

You can share this post!

Wazee wamfanyia kidosho tambiko kwa kutusi nyanya mkwe

Raila atua Uingereza kuosha tope la Ruto

T L