Habari za Kitaifa

Walimu wa JSS wasitisha mgomo wao

June 8th, 2024 1 min read

NA WINNIE ATIENO

MAELFU ya walimu wa Shule ya Sekondari Msingi (JSS) ambao wamekuwa kwenye mgomo tangu Aprili 17, 2024, wamesitisha kampeni hiyo hadi Julai 5, 2024.

Walimu hao wanagenzi waliamua kusitisha mgomo wao ili kutoa nafasi kwa Bunge la Kitaifa kupitisha bajeti mnamo Alhamisi.

Walimu hao 46,000 wanataka mikataba ya kudumu (PnP).