Habari za Kitaifa

Walimu wa JSS wasitisha mgomo

June 1st, 2024 1 min read

NA MWANDISHI WETU

WALIMU wa Sekondari Msingi (JSS) wamesitisha mgomo wa wiki mbili baada ya kutia saini makubaliano ya kurejea kazini.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Masilahi ya Walimu wa Sekondari na Vyuo (Kuppet) Akello Misori alisema Jumamosi kwamba walikubaliana na Tume ya Kuajiri Walimu Nchini (TSC) ambayo iliahidi kuwaajiri walimu hao kwa mkataba wa kudumu (PnP) katika mwaka ujao wa kifedha.

Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC ni Dkt Nancy Macharia. TSC imeondoa barua za kuwaonya walimu, ilizokuwa imewatumia ikitishia kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Soma Pia: Mgomo wa walimu wa JSS wazaa matunda Bunge likisema waajiriwe