Habari Mseto

Walimu wa vyuo kupimwa corona

July 7th, 2020 1 min read

GEORGE MUNENE na FAUSTINE NGILA

Walimu wote wa vyuo vya kiufundi watalazimika kupimwa virusi vya corona kabla ya kufunguliwa kwa shule, amesema Waziri wa Elimu Prof George Magoha.

Prof Magoha alisema Jumapili kwamba ndipo wanafunzi wawe salama lazima walimu wawe wamepimwa corona na kuthibitishwa hawana virusi hivyo.

Alisema kwamba Kenya ina zaidi ya walimu 130,000 alipokuwa akiongea akiwa Kenya School of Government kaunti ya Embu.

Aliagiza walimu wapimwe wiki mbili kabla ya shule kufunguliwa.

Prof Magoha aliekeza Katibu wa Elimu Belio Kipsang kuhakikisha kwamba shughuli hiyo imeendea ipasavyo kabla ya vyuo vya ufundi  kufunguliwa.

“Tunapaswa kuwa makini kabla ya shule kufunguliwa,” alisema.

“Kupimwa virusi vya corona itakua mtindo wanafunzi watakapo jerea shuleni,” alisema.

Waziri huyo aliongeza kwamba shule zitafunguliwa pale serikali itakuwa na uhakika kwamba mikakati imewekwa shuleni ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wako salama.