Walimu wakosa chanjo ya corona kituoni

Walimu wakosa chanjo ya corona kituoni

Na ALEX NJERU

MAMIA ya walimu katika Kaunti ya Tharaka Nithi waliorauka kupewa chanjo ya Covid-19 kabla ya muda wa makataa kukamilika walishtuka kugundua dozi hizo zilikuwa zimeisha.

Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) ilikuwa imewapa walimu kutoka shule za umma na za wamiliki binafsi makataa ya siku saba kupokea dozi kamili ya chanjo hiyo la sivyo wachukuliwe hatua za kinidhamu ambazo hazikufafanuliwa.

Idadi kubwa ya walimu walisema wamekuwa wakizuru hospitali mbalimbali kwa muda wa wiki moja lakini hawakuweza kupata chanjo kwa sababu ya foleni ndefu na ukosefu wa dozi hizo katika baadhi ya vituo vya afya.

Waziri wa Afya katika Kaunti ya Tharaka Nithi, Dkt Gichuyia Nthuraku, alisema watu zaidi ya 2,000, wengi wao wakiwa walimu na watumishi wa umma, walipokea chanjo wiki iliyopita na kumaliza dozi walizokuwa nazo.

Hata hivyo, alisema wanatarajia kupokea dozi zaidi kufikia Jumatano wiki hii.

Wizara ya Afya ilipokea chanjo kadhaa Jumapili.

You can share this post!

Taliban wawapa wanajeshi wa Amerika siku 7 waondoke

Faini Sh10,000 au jela kutema mate jijini