Walimu waunga azma ya Wanga kuwania ugavana

Walimu waunga azma ya Wanga kuwania ugavana

NA GEORGE ODIWUOR

AZMA ya Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Homa Bay Gladys Wanga (pichani) ya kuwania ugavana wa Homa Bay, imepigwa jeki baada ya maafisa wa Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri (Kuppet), kumuunga mkono.

Katibu Mkuu wa Kuppet, Bw Akelo Misori, ambaye pia alikuwa akiwania ugavana, alisema Bi Wanga ana nafasi nzuri ya kuchaguliwa gavana katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 na akatoa wito kwa walimu kumuunga mkono.

Bw Misori ni miongoni mwa wanasiasa 10 ambao walikuwa wametangaza nia ya kuwania kiti cha ugavana wa Homa Bay.

Lakini kiongozi wa ODM Raila Odinga aliingilia kati na kuwashauri wagombeaji wengine kujiondoa ili wampishe Bi Wanga.

Baadaye Mbunge huyo Mwakilishi wa Kike alimteua aliyekuwa mbunge wa Kasipul Oyugi Magwanga kuwa mgombea mwenza wake.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Afya ya uzazi kuhusu fistula itengewe pesa na...

Pigo kwa Chris Wamalwa kambi ya Natembeya ikipigwa jeki

T L