Habari Mseto

Waliniombea nife nilipougua corona – Gavana

October 6th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Gavana wa Kaunti ya Tana River Godhana Dhadho kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu alivyojipata na virusi vya corona.

Gavana huyo ambaye alipatikana na virusi vya corona mwezi Agosti alisimulia jinsi virusi hivyo vilivyomwathiri huku akielezea wakazi wa Hola kuhusu mazunguzo na jumbe kutoka kwa marafiki za kusitikisha.

Alipopatikana na virusi vya corona walinzi wake pamoja na wafanyakazi wake walilazimika kuishi naye nyumbani kwake. Kulingana na mkuu huyo wa kaunti, ugonjwa huo ulianza kwa dalili za kuumwa na kichwa na homa.

Wakati huo huo marafiki wake watatu walikuwa wameripotiwa kuwa wanaugua virusi vya corona huku wengine wakiwa wamelazwa kwenye chumba cha watu mahututi.

Hakuna mmoja wa maafisa wake wa usalama ambaye alionyesha dalili zozote za virusi vya corona wakati huo.

“Inaonyesha kwamba virusi hivyo vilitupata kitambo na tulikuwa tunatembea vikiwa mwilini kwani dalili za  kwanza zilijionyesha kwangu. Wafanyakazi watu walitengwa na matibabu  yakaanza mara moja,” alisema.

Afisi yake iLifungwa baada ya wafanyakazi wake kupatikana na corona. “Sijui nilitoa virusi hivyo wapi nilikuwa makini sana kuakikisha kwamba nafuata maagizo ili kujikinga na kupata virusi vya corona lakini bado ilinipata,” alisema..

Alipokuwa hospitalini, gavana huyo alisema kwamba aligundua watu wengi walikuwa wanamuombea afariki baada ya kupata habari kuhusiana na hali yake ya kiafya.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA