Kimataifa

Waliohusika kwa mauaji ya halaiki Rwanda wakamatwa

October 7th, 2020 1 min read

NA AFP

Wanaume watatu wanaoaminika kuwa wahusika kwenye mauaji ya halaiki ya watu nchini Rwanda mwaka wa 1994 wamekamatwa na kushtakiwa kwa kukiuka haki za binadamu, imesemaa afisi ya mwendesha mashtaka.

Afisi hiyo haiktoa taarifa zaidi kuhusiana na watatu hao lakini habari zaidi kuwahusu zitapatikana kupitia wa kwa mashahidi na upelelezi wa taifa la Belgium.

“Wawili walikamatwa Jumanne jijini huku mwenzao wa tatu akikamatwa kwenye mkoa wa Hainault,” alisema Erick Van Duyse msemaji wa afisi ya mashtaka ya Belgium.

“Watatu hao walishtakiwa kwa udhalilishaji wa bindamu na kukiuka kwa haki za binadamu ,”alisema msemaji huyo.

Mmoja wao anachunguzwa kupitia njia za kielekroniki huku wengine wawili wakiwa wamezuliwa.

Mauaji hayo yaliyotokea 1994 yaliacha watu 800,000 wakiwa wamefariki sanasana Tutsi na Hutu wachache.

Mwaka jana Desemba afisa mkuu wa Rwada Fabian Neretse alipatikana na hatia ya mauaji hayo na kufungwa miaka 25 gerezani.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA