Habari Mseto

Walioiba mamilioni ya sacco kidijitali wanaswa

November 14th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Watu watatu waliosemekana kuingilia mfumo wa Habari na Teknolojia wa vyama vya ushirika (Sacco) na kuiba mamilioni wamekamatwa Nairobi, katika eneo la Dagoretti.

Kulingana na afisi ya uchunguzi wa kihalifu (DCI), watatu hao Wakenya Zahra Ahmed na Mr Abdullazac Rajab na Patrick Emmanuel Gabantu kutoka Uganda, walihojiwa Jumatano na walitarajiwa kushtakiwa siku hiyo.

Baadhi ya Sacco zilizotapeliwa ni Safaricom, Bamburi, Stima na zingine kulingana na ujumbe uliowekwa Twitter na DCI.

Hayo yalitokea huku vyama vya ushirika vikitakiwa kuimarisha usalama wa mifumo yao ili kukabiliana na kuingiliwa hivyo.

Kulingana na ripoti ya awali ya shirika la uchunguzi kuhusu usalama wa matumizi ya mifumo ya kidijitali, Sh17 bilioni ziliibwa na watu wa kuingilia mifumo mwaka wa 2016.