Habari Mseto

Waliojifanya DCI wabambwa

September 1st, 2020 1 min read

 Na Hilary Kimuyu

Wapelelezi kutoka kitego cha DCI waliwakamata watu wawili Jumatano jioni waliokuwa wanajifanywa kuwa maafisa wa DCI.

Wawili hao, Dennis Moturi Nyakundi na Victor Omare Onsare walikamatwa wakiwa kwenye hoteli moja Nairobi baada ya mahojiano na mbunge mmoja kupitia mtandao wa kijamii.

Walikuwa wametumia mbunge huyo notisi gushi huku wakimuomba  afike kwenye makao makuu ya DCI  kuonjiwa kuhusuina na jambo ambalo hawakulitaja ,ujumbe wa DCI ulisema.

Mbunge huyo alipigiwa na namba binafsi ikisema kwamba mkutano huyo umehamiishwa kutoka  makao makuu ya DCI hadi kwa hoteli.

Kulingana na ujumbe wa DCI wawili hao walikamtwa walipokuwa wakimgoja mbunge huyo ambaye hakutajwa jina.

“Mbunge huyo alishuku kuwa watu hao hawakuwa DCI na akaripoti jambo hilo kwa DCI  hapo ndipo wawili hao waliwekewa mtengo na mwishowe wakakamatwa.

Tafsiri na Faustine Ngila