Habari Mseto

Waliomuua bawabu wakamatwa

August 1st, 2020 1 min read

GEORGE MUNENE na FAUSTINE NGILA

Polisi Kirinyaga wamekamata washukiwa watatu kuhusiana na mauaji ya bawabu mmoja.

Washukiwa hao walikamatwa baada ya polisi kuvamia waliokuwa wahuni hao waliokuwa wamejificha Ijumaa jioni kwenye mji wa Kutus.

Kamanda wa polisi wa Mwea Mashariki alisema kwamba watatu hao watashtakiwa kwa mauaji baada ya uchunguzi kukamilika.

Bawabu huyo alipigwa hadi kifo huku mwingine akipata maumivu mabaya Jumatatu usiku kwenye wizi wa wa mabavu eneo ya Ndomba.

Aliyeponea mashambulizi hapo alilazwa kwenye hospitali ya rufaa ya Kerugoya akiwa kwenye hali mbaya

Mabawabu hao walishambuliwa wakati wezi hao walishambulia eneo ya ujenzi ya maji taka ya Ndomba.

Wakazi walisema kwamba wezi hao walifanya kitendo hicho cha untyama saa tisa usiku.

Mabawabu hao walijaeribu kujiokoa lakini wakashidwa nguvu na majambazi hao

Wezi hao waliiba vifaa vya ujenzi ,betri za gari na bidhaa zingine za dhamna ya maelfu,alisema polisi.