Habari Mseto

Waliotoweka wiki tatu zilizopita bado wasakwa

October 21st, 2020 1 min read

NA ERIC MATARA

Ni wiki tatu sasa baada ya kupotea kwa ndugu wawili waliokuwa wakiishi Nakuru na bado polisi hawajapata fununu zozote kuhusiana na mahala walipo.

Wawili hao Joseph Machari wa miaka 39 na Moses Kamau mwalimu wa shule ya Kijabe wa miaka 37 aliyekuwa mfanyabiashara walipotea Septemba 21. Bw Kamau  alikuwa na duka la kielekroniki mjini Nakuru.

Wapeleezi kutoka kitego cha DCI wanajaribu kutafuta habari kuhusiana na kupoteaa kwa wawili hao.

Mpelelezi mkuu aliambia Taifa Leo kwamba simu zao zilizimwa karibu na Nakuru Golf Club kinachopakana na msitu wa Menengai.

“Simu ya Kamau ilikuwa imewashwa saa saba unusu mchana Septemba 21, ya Macharia ilizimwa dakika chache baadaye. Tunaendelea kutafuta habari zinazotusaindia kuwwattafuta,” alisema mpelelezi huyo.

“Tuligundua kwamba wawili hao walikula chakula cha mchana kwenye hoteli ya Shemeji kabla ya kufika kilabu cha Nakuru Golf,” alisema mpelezi mwingine.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA