Wamrai Rais asaidie kutatua mzozo wa ardhi waliyorithi

Wamrai Rais asaidie kutatua mzozo wa ardhi waliyorithi

Na GEORGE MUNENE

WAKAZI wa Mbeere Kusini katika Kaunti ya Embu, wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta, kusaidia kutatua mzozo wa muda mrefu unaohusu kipande cha ardhi chenye ekari 54,000, kinachozingirwa na utata.

Wakizungumza katika soko la Ndune, eneo la Makima, waliwashutumu watu na mashirika maarufu dhidi ya kujaribu kuwafurusha kutoka kwa ardhi waliorithishwa na mababu zao ya Mwea Trust Land.

Wakiongozwa na diwani wa eneo hilo, Bw Philip Nzangi, wakazi hao walimsihi Rais awaokoe wasije wakafurushwa na wanyakuzi hao wa ardhi na mashirika ya mabwenyenye ikiwemo kuhakikisha mgogoro huo unasuluhishwa kikamilifu.

 

You can share this post!

Fujo shuleni: Walimu wakuu Nyandarua kushtakiwa

Katibu mkuu kushtakiwa kwa kumtandika mke kwasabaabu ya...

T L