Habari Mseto

Wamuua mwanamke licha ya onyo la wazee

October 8th, 2020 1 min read

NA BRIAN OCHARO

Baada ya kulemewa kulipa faini waliyotozwa na wazee ya Sh33,000 kwa uhuni, Garama Mboko na mwenzake waliamua kumuua rafiki  yao mwanamke na kutupa mwili msituni.

Kwenye ushahidi uliotolewa kortini, wawili hao walimteka nyara mwanamke mmoja nyumbani kwake na kumpeleka kwenye msitu wa Mirima, Gaze, Kilifi ambapo walimuua kutokana na mzozo wa kimapenzi.

Wanaume hao wawili walipatikana na mausiano haramu na mwanamke huyo, lakini jambo hilo lilitatuliwa na wazee na wakakwapa faini ya Sh10,000 na ingine ya Sh13,500 kwa kuingia nyumbani kwa mwanamke huyo.

Mwenzake ambaye walitendea unyama huo hakutajwa jina mahakamni lakini aliachiliwa kwa dhamana ya Sh20,000.

Jamaa za mwanamke huyo walisema kwamba wanaume hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo uliowafanya wafikishwe mbele ya wazee.

Shahidi mmoja alisema kuna wakati Mbokoa limtishia mwathiriwa. Kisa hicho kilipotiwa kwa chifu wa eneo hiloambaye alitatua mzozo huyo na kuangiza mwanaume huyo kulipa faini kwa kumtishia mwanamke huyo.

Lakini viongozi hao walishindwa kutatua mzozo huo baada ya Bw Mboko kutishia kumuua mwanamke huyo tena kwa panga.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA