Habari Mseto

Wanafunzi 38 waptikana na corona Baringo

November 15th, 2020 1 min read

FLORAH KOECH NA FAUSTINE NGILA

Zaidi ya wanafunzi 38 wa kidato cha nne kutoka Shule ya Upili ya Kabarnet wamepatikana na virusi vya corona, kamishena wa Kaunti ya Baringo Henry Wafula amethibitisha.

Kulingana afisa huyo sampuli 48 zilipimwa baada ya mwanafunzi mmoja kupatiana na virusi vya corona wiki iliyopita.

Ripoti zilisema kwamba wanafunzi 48 ndio walipimwa ati ya wanafunzi 254 wa kidato cha nne.

“Ni ukweli kwamba mwanafunzi mmoja wa shule ya upili ya Kabarnet alipatikana na virusi vya corona iliyoelekea Wizara ya afya kupima wanafunzi wengine 48 aliotangamana nao huku 38 wakipatikana na virusi vya corona Jumamosi ,”alisema Bw Wafula.

Alisisitiza kwamba shule hiyo haitafungwa ata kama kuna virusi vya corona huku akisema kwamba wanafunzi walioathirika watatibiwa kwenye chumba kimoja kilichotengwa cha kulala humo shuleni.

“Hatutafunga shule tumeweka wanafunzi ambao wameathirika kweenye chumba kimoja ambapo watatibiwa,”aliogeza.

Kamishena wa Kaunti aliambia Taifa Leo kwamba mikakati imewekwa na idara ya maswala ya afya ya Kaunti hiyo ili kunyunyuzia dawa shule hiyo mabyo iko mjini Kabarnet na hakuna yeyote atakaye ruhusiwa kuingia shuleni humo.

Alisema piawalimu shuleni humo wamepimwa na kuna mikakati iliyowekwa kuakikisha kwamba wafanyakzi wengine hapo shuleni wamepimwa pia.