Habari Mseto

Wanafunzi na walimu waugua corona Siaya

November 11th, 2020 1 min read

NA DICKENS WASONGA NA FAUSTINE NGILA

Wanafunzi wawili na walimu watatu wamepata  virusi vya corona, Idara ya Elimu ilitangaza Jumamosi Kaunti ya Siaya.

Mkurugenzi wa elimu  wa kaunti Joseph Wamocho alisema kwamba pia wafanyakazi wa shule ya sekondari walikuwa wameathirika.

Kati ya shule zilizoathirika ni shule ya upili ya Maranda Kaunti ndogo ya Bondo ambapo wanafunzi 11 wameathirika ,shule ya msingi ya Central na Siaya Town ship ambazo ziko Alego-Usonga pamoja na shule  ya sekondari ya Nyamninia..

Kisa cha shule ya Central ni cha mwanafunzi na Nyamninia ni mwalimu.

Walimu wengine wawili walioathirika ni wa shule ya upili ya Siger.

“Kesi mbili za shule ya upili ya Township ni za wafanyakazi wa shule ,”alisema Bw Wachomohuku akiogeza  kwamba wanafunzi wa Maranda wanaendelea kutibiwa kwenyee hospitali ya Bondo.