Habari Mseto

Wanafunzi wafika shuleni kupata kuku madarasani

October 12th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mwea Brethren, Kaunti ya Kirinyaga walipigwa na butwaa Jumatatu walipofika shuleni na kupata madarasa yamejaa kuku.

Mmiliki wa shule hiyo alifanya shule hiyo kuwa shamba la kufuga kuku wakati serikali ilifunga shule mwezi Machi wakati janga la corona lilizuka.

Wanafunzi hao walifika shuleni wakiwa tayari kusoma lakini wanakutana na kuku waliokuwa wakilishwa na usimamizi wa shule hiyo ili kulipa madeni.

Usimamizi wa hule hiyo ulilazimika kuondoa baadhi ya kuku ili wanafunzi wapate nafasi ya kusomea.

“Tulilazinika kutoa kuku wengine kutoka kwa darasa linguine ili kupata nafasi ya wanafunzi wa darsa la nne ambao walikuwa wa kwanza kufika shuleni kurejelea masomo,” ulisema usimamizi wwa shule.

Bi Maina alisema kwamba ni bahati mbaya kwamba serikali iliruhusu wanafunzi kurudi shuleni kabla ya kuku hao kukomaa.

Aliogeza kwamba shule hiyo inakumbwa na changamoto ya nafasi ya kusomea lakini itabidi wanafunzi wavumilie kwanza.

“Itatuchukua muda kutoka huku hawa hapa kwani hawajakomaa kwa ajili ya kuuzwa,”alisema..

Alisema kwamba wakiwa na mumewe walilazimika kufuga kuku ili walipe mkopo waliokuwa wamechukua kutoka kwa benki.

Alieleza kwamba walilazimika kuuza gari lao ili waweze kuanzisha mradi huo wa kufuga kuku.