Wanafunzi wanaoshukiwa kupanga kuchoma shule kuzuiliwa zaidi na polisi

Wanafunzi wanaoshukiwa kupanga kuchoma shule kuzuiliwa zaidi na polisi

MERCY MWENDE na GEORGE MUNENE

WANAFUNZI kumi na moja wa shule za sekondari za Kagumo na Kiandu wanaoshtakiwa kwa kujaribu kuchoma shule zao, wataendeleza kuzuiliwa na polisi hadi Jumatano, mahakama ya Nyeri imeagiza.

Akitoa agizo hilo jana, Hakimu Mkuu Mkuu Mwandamizi James Macharia, alisema wanafunzi hao hawakuweza kujibu mashtaka kwa kuwa hawakuwa na mawakili. Wanafunzi watatu kutoka Kigumo wanalaumiwa kwa kupanga njama ya kuchoma sehemu ya shule Jumapili ya Novemba 7 mwendo wa saa mbili usiku.

Kulingana na karatasi ya mashtaka iliyowasilishwa kortini, wanafunzi hao walipatikana na nusu lita ya mafuta ya taa na kiberiti miongoni mwa vifaa vingine katika hali iliyoonyesha kwamba walikuwa wakipanga kutekeleza uhalifu.

Nao wanafunzi wanane kutoka shule ya sekondari ya Kiandu wamelaumiwa kwa kujaribu kuchoma jengo la kidato cha kwanza na vyoo vya shule hiyo mnamo Novemba 3 saa mbili usiku. Walipofikishwa kortini, wanafunzi hao walisema kwamba shule zao hazikufanya uchunguzi wa kina na hazikuwapata waliohusika.

Wale wa shule ya sekondari ya Kagumo walisema kwamba walisingiziwa na wanafunzi wenzao japo walikiri kwamba wanawafahamu waliohusi

You can share this post!

Serikali yatoa Sh450 milioni zaidi ya kuiokoa mifugo

Shirika lataka sera za wahudumu melini

T L