Wanafunzi waonywa dhidi ya mimba za mapema wakiwa likizoni

Wanafunzi waonywa dhidi ya mimba za mapema wakiwa likizoni

Na SAMMY KIMATU

WATOTO wameshauriwa kuepukana na marafiki wanaoweza kuwaigiza kwa mambo mambaya kama vile kutumia mihadarati, vileo na masuala mengine kama vile ndoa za mapema na mimba zisizotakikana.

Wazazi nao wameulizwa kuwatayarisha wanao kujiunga na kidato cha kwanza mwakani badala ya kutumia pesa nyingi kwa ajili ya sikukuu ya Krisimasi na Mwaka Mpya.

Hayo yalitamkwa jana na Mwakilishi wa Wodi ya Mutituni katika Kaunti ya Machakos, Bw Yohana Munyao.

Mwanasiasa huyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwatuza wanafunzi na kufunga shule kwa likizo ya Disemba katika Johns Baraka Academy iliyo katika wodi yake.

“Mimba za wanafunzi wa kidato cha kwanza na kuwacha shule hutokana na kuchagiwa kwa jinsi mtoto alivyoitumia likiozo ya Disemba punde anapomaliza mtihani,” Bw Munyao akasema.

Fauka ya hayo, aliwahimiza wenyeji kutayarisha mashamaba mapema kwa ajili ya mvua kwa kupanda mapema, kupata ushauri wa wataalamu wa kilimo kuhusu mbegu zile nzuri na mbolea badala ya kasumba ya kufanya mambo kwa kujaribu wakikosea na kutumia njia za kitamaduni za kilimo zilizopitwa na wakati.

You can share this post!

Ununuzi wa umeme wasimamishwa kurekebisha bei

Afanya KCPE akiwa ndani baada ya kuchoma nyumba ya mamake

adminleo