Habari Mseto

Wanafunzi wazidi kuugua corona Mombasa

October 28th, 2020 1 min read

Na Winnie Atieno

Wananfunzi 22 wamepatikana na virusi vya corona kaunti ya Mombasa tangu shule zifunguliwe, walisema maafisa wa afya Jumanne.

Wiki iliyopita serikali ya Kaunti ya Mombasa ilifanya vipimo vya walimu na wanafunzi baada ya shule kufunguliwa.

Shule ya upili la Tononoka ilirekodi visa 16 huku mwalimu mkuu akifariki kutokana na virusi vya corona Jumatatu.

Shule ya upili ya Star of the Sea pia ilirekodi visa vya corona baada ya sampuli 156 kufanyiwa vipimo.

Mkurugenzi wa maswala ya afya kaunti ya Mombasa Dakatari Salma Swaleh aliwaomba wakazi waendelee kufuata mikakati iliyowekwa na ya serikali.

Tangu kisa cha kwanza kuripotiwa kaunti ya Mombasa imeripoti visa 897 vya maafisa wa afya ambao walipata virusi vya corona na kifo kimoja kinachohusishwa na virusi vya corona cha afisa wa afya. Idadi ya vifo kaunti hiyo imesfika 93 huku visa vya corona vikiwa 3,693 kufikia Oktoba 25 kwa sampuli 63,673 zilizopimwa,” alisema Dkt Swaleh.

Ugonjwa huo wa corona umekithiri sana maeneo ya kisiwani hili likileta hofu kati ya wakazi na maafisa wa afya.

Wiki iliyopita mwenyekiti wa kamati ya kushughulikia maswala ya corona Gilbert Kitiyo alikutana na wadau kutoka sekta ya afya kuzungumzia maswala ya kudhibiti corona.