Wanajeshi 23 waliofungwa kwa mauaji ya Kabila waachiliwa baada ya miaka 20

Wanajeshi 23 waliofungwa kwa mauaji ya Kabila waachiliwa baada ya miaka 20

Na Mashirika

WANAJESHI 23 walioshtakiwa kwa tuhuma za kushiriki kwenye mauaji ya aliyekuwa rais wa DR Kongo, Laurent Kabila, wameachiliwa huru baada ya kukaa gerezani kwa karibu miongo miwili.

Rais Kabila aliuawa kwa kupigwa risasi na mmoja wa walinzi wake mnamo 2001.Mamia ya wanajeshi walifungwa gerezani kufuatia kesi iliyofuata, miongoni mwao akiwemo Kanali Eddy Kapend, ambaye alihudumu kama msaidizi wake wa kibinafsi.

Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yalikashifu jinsi kesi hiyo ilivyoendeshwa.Baadhi ya watu walisema wanajeshi wengi waliohukumiwa hawakuwa na hatia.

Mwanawe Kabila, Joseph Kabila, alikataa miito ya kuwasamehe wanajeshi hao, alipohudumu kama rais.Kuachiliwa kwa wanajeshi hao kunajiri wakati kuna mvutano mkali wa kisiasa kati ya Kabila na Rais Felix Tshisekedi.

 

You can share this post!

Magufuli ampongeza waziri wa China kwa kutovaa maski

DINI: Matunda ya kesho yako kwenye mbegu za leo kwa hivyo...