Wanajeshi wa Uganda wamzima balozi wa Amerika kumtembelea Bobi Wine

Wanajeshi wa Uganda wamzima balozi wa Amerika kumtembelea Bobi Wine

MASHIRIKA NA WANGU KANURI 

Balozi wa Amerika nchini Uganda alizuiwa kumtembelea kiongozi wa upinzani Bobi Wine nyumbani mwake na wanajeshi Jumanne. Balozi huyo alisema kuwa amri hiyo ya kumfungia Wine nyumbani mwake chini ya ulinzi ni ishara inayoogofya.

Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amefungiwa nyumbani mwake chini ya ulinzi makli tangu Alhamisi punde tu baada yake kupiga kura katika uchaguzi wa urais nchini humo.

Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, ambaye amekuwa uongozini tangu 1986, alitangazwa kama mshindi kwa kura asilimia 59 dhidi ya Wine aliyekuwa na kura za asilimia 35.

Balozi huyo Natalie E. Brown alikuwa ananuia kuangalia usalama na afya ya Wine alipozuiwa mnamo Jumatatu. Hata hivyo, msemaji wa serikali Ofwono Opondo alidinda kuchukua simu ili kutoa maoni kulingana na tukio hilo.

Kama ulivyosema ubalozi, upigaji kura wa wiki iliyopita ulikuwa wenye unayanyasaji kwa wagombeaji wa upinzani, ukandamizaji wa vyombo vya habari na watetezi wa haki pamoja na kuzimwa kwa intaneti nchini.

“Matendo haya yasiyo ya kisheria na kufungiwa nyumba chini ya ulinzi kwa mgombezi wa urais kunaendelea kutia wasiwasi kwa demokrasia ya Uganda,” ubalozi ukasema.

Hali kadhalika, Amerika na Muungano wa Ulaya hawakuwapeleka misheni wa kuangalia upigaji wa kura kwa sababu ya kutopewa vibali na kudorora kwa serikali ya Uganda kwa kutotekeleza mapendekezo ya misheni zilizopita.

Wakati wa kampeni, vikosi vya usalama mara kwa mara vilisambaratisha mikutano ya kisiasa ya umma ya Wine kwa vitoa machozi, risasi, kuchapwa na kutiwa nguvuni. Walieleza sababu ya kutumia nguvu ili kuwa kwa sababu mikutano hiyo ilienda kinyume na sheria zilizowekwa ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.

Mnamo mwezi wa Novemba, watu 54 waliuliwa na vikosi hivyo vya usalama baada ya waandamanaji kulalamikia kutiwa mbaroni kwa Wine kwa kudaiwa kukiuka vidokezo vya kuzuia uenezi wa Corona.

Wine na chama chake National Unity Platform (NUP) wamekataa matokeo ya uchaguzi na wakasema kuwa wanapangia kufika kortini.

Jumatatu vikosi vya usalama vilizuia wanachama kufika ofisini katika mji mkuu, huku chama kikisema kuwa jambo hilo linatatiza juhudi zao za kukusanya ushahidi wa kuonyesha kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki.

You can share this post!

Wakongwe wanavyoangamia wakimumunya raha ya dunia

Tangatanga watimua wahubiri na kuteka mazishi ya diwani