Wanaolengwa na chanjo ya crorona waingiwa na hofu

Wanaolengwa na chanjo ya crorona waingiwa na hofu

Na Mwangi Muiruri

UTOAJI chanjo ya virusi vya corona katika Kaunti ya Murang’a imekumbwa na shaka na uoga wa wanaolengwa.

Licha ya Gavana Mwangi wa Iria kuchanjwa hadharani na kutangaza kuwa hii chanjo ya AstraZeneca iko shwari, baadhi ya wananchi wakiweno wauguzi, walimu na maafisa wa polisi waliambia Taifa Leo kuwa wanahitaji muda zaidi kabla waamue kupewa chanjo.

‘Suala la kuwekwa viini ndani ya mwili ili kutoa kinga inafaa kutanguliwa na ukaguzi mkuu wa kiafya na vipimo vya kina vifanywe ili kubaini uthabiti wa mwili wa kupokea viini geni na kuishi navyo. Hili si jambo la kukimbiliwa,” akasema muuguzi aliyeomba kutotajwa gazetini.

Bw James Kamande ambaye alijitokeza kushuhudia chanjo hiyo ikizinduliwa alisema kwamba bado hana uhakika kuwa anafaa kuchanjwa wakati wake ukifika.

Serikali kuu kwa upande wake kupitia Waziri wa Afya Bw Mutahi Kagwe imekuwa ikisisitiza kuwa chanjo ni salama na imepitishiwa vigezo vya kina vya ukaguzi na kuaminika kuwa haitakuwa na madhara yoyote kwa watakaochanjwa.

Hii ni licha ya kuwa imesitishwa katika mataifa mengi yakiwemo ya Ulaya na Afrika Kusini.

You can share this post!

Wakazi walaani polisi kuwatesa Mama Ngina

Kesi ya kumpinga Kavindu kuanza leo