Wanaraga Kenya Lionesses warushwa nafasi tatu hadi 28 duniani

Wanaraga Kenya Lionesses warushwa nafasi tatu hadi 28 duniani

Na GEOFFREY ANENE

Kenya imetupwa chini nafasi tatu hadi nambari 28 kwenye viwango bora vya Shirikisho la Raga Duniani vya kinadada vilivyotangazwa hapo Agosti 31.

Hii ni baada ya timu ya Kenya maarufu kama Lionesses kupigwa na Colombia 16-15 katika mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2021 ugani Nyayo jijini Nairobi hapo Agosti 25.

Vipusa wa kocha Felix Oloo sasa wanakamata nafasi ya tatu barani Afrika nyuma ya Afrika Kusini inayosalia 13 duniani na Cameroon iliyorukia nafasi ya 25 duniani kutoka 26.

Colombia inapatikana katika nafasi ya 26 baada ya kuimarika kutoka nafasi ya 30. Zambia ni ya nne Afrika baada ya kuteremka nafasi moja.

Kabla ya kuvaana na Colombia, Lionesses walipoteza mechi nne za kupimana nguvu. Walichapwa na Madagascar 27-15 Julai 3 na 10-0 Juli 11 ugani Nyayo halafu wakapoteza 66-0 Agosti 12 na 29-22 Agosti 16 dhidi ya wenyeji Afrika Kusini mjini Stellenbosch.

Kenya ilipata tiketi ya kumenyana na Colombia baada ya kumaliza Kombe la Afrika 2019 katika nafasi ya pili nyuma ya Afrika Kusini na juu ya Uganda na Madagascar. Colombia, ambayo itashiriki mashindano ya mwisho ya kuingia Kombe la Dunia 2021 litakaloandaliwa mwisho wa mwaka 2022 nchini New Zealand, ilipata tiketi ya kuchuana na Kenya ilipoibuka mshindi Afrika ya Kusini.

  • Tags

You can share this post!

Ashtakiwa kutisha kuua mwanamke kwa kukataa uchumba

Okutoyi aanza tenisi ya J2 Cairo kwa ushindi