Wanasiasa wakuu watatii kanuni au wataendelea kupepeta corona?

Wanasiasa wakuu watatii kanuni au wataendelea kupepeta corona?

BENSON MATHEKA Na WINNIE ONYANDO

WAKENYA wanasubiri kuona ikiwa vigogo wa kisiasa nchini wataahirisha mikutano yao ya kisiasa waliyopanga maeneo tofauti nchini kuanzia wikendi hii baada ya serikali kusitisha hafla hizo kama njia ya kudhibiti msambao wa corona.

Ijumaa, Inspekta Jenerali wa polisi Hillary Mutyambai alionya wanasiasa dhidi ya kuandaa mikutano ya aina yoyote nchini akisema, ameagiza maafisa wake kutekeleza kikamilfu kanuni za Wizara ya Afya.

Akizungumza akiandamana na waziri wa afya Mutahi Kagwe jijini Nairobi, Bw Mutyambai alisema hakuna atakayeruhusiwa kukiuka kanuni hizo.

“Idadi ya maambukizi inaendelea kupanda. Tukiendelea na hafla za kisiasa, basi tutamalizwa na janga hili,” alisema Bw Kagwe akitoa taarifa kuhusu hali ya corona nchini nje ya Afisi ya Rais, Harambee House, Nairobi

Hata hivyo imeibuka kuwa wanasiasa ambao wamekuwa wakipuuza kanuni hizo na kuchangia ongezeko la maambukizi nchini, wamepanga mikutano kuanzia wikendi hii.

Ijumaa, viongozi wa eneo la Magharibi walisema wamekamilisha maandalizi ya ziara ya Rais Uhuru Kenyatta katika eneo hilo.

Mnamo Jumanne, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga alitangaza yeye na washirika wake wa kisiasa wataandaa mikutano kaunti ya Kisii, Kakamega, Pwani na eneo la Mashariki ya Mlima Kenya kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Naibu Rais William Ruto amepanga mikutano kaunti za Mashariki mwa Mlima Kenya.

Katika ziara hiyo, anatarajiwa kutembelea maeneobunge mawili – Mbeere Kusini na Runyenjes – ambapo ataendeleza kampeni yake ya hasla, kuhudhuria hafla za kanisa, kufanya mikutano ya barabarani, na kisha kupata habari kuhusu shughuli ya kuandikisha wanachama wa chama cha United Democratic Alliance (UDA).

You can share this post!

Msimu wa talaka

Corona: Kagwe atoa afueni kwa kaunti 13 za magharibi mwa...