Habari MsetoSiasa

Wanasiasa wataka viwanda vijengwe katika shamba la Del Monte

August 8th, 2020 2 min read

Na MWANGI MUIRURI

WABUNGE watano kutoka Kaunti za Murang’a na Kiambu sasa wanaitaka serikali ihakikishe imezindua mradi wa viwanda katika shamba linalotarajiwa kutengwa kutoka miliki ya kampuni ya Marekani iliyoko Mjini Thika, Del Monte.

Mradi huo walisema unafaa uwe na muundo wa Export Processing Zone (EPZ) ulio na uwezo wa kutoa nafasi zisizopungua 10, 000 za ajira kwa wenyeji.

Kampuni hiyo ya utemgenezaji juisi hasa za mananasi humiliki takriban ekari 22, 000 na ambazo kwa sasa zionabishaniwa na wenyeji wa Kaunti hizo mbili kutengwe angalau asilimia 30 yazo kuwafaa. Mzozo huo wa umiliki umesababisha kuzuka kwa kizungumkuti kuhusu kutolewa kwa hatimiliki ya kuendeleza mkataba wa Del Monte na Serikali ya Kenya kuhusu shamba hilo.

Hapo jana, wabunge Nduati Ngugi wa Gatanga, Jude Njomo wa Kiambu Mjini, Patrick Wainaina akiwakilisha Thika Mjini, Wainaina King’ara wa Ruiru na Mary wa Maua wa Maragua walisema kuwa usoroveya unafaa kutekelezwa mara moja na ekari kamili zinazofaa kuwa katika umiliki wa Del Monte zibainike na hatimaye hatimiliki itolewe.

“Del Monte haina shida yoyote na hali kwamba inafaa kutenga ekari kadha za kutumika kwa manufaa ya wenyeji…Tayari, hii ni kampuni ambayo imedhihirishia taifa hili kwamba ni rafiki wa dhati kwa kuwa imewapa ajira zaidi ya vibarua 6, 000 na ambao huzoa Sh2.5 bilioni kama mishahara kwa mwaka,” wakasema katika taarifa ya pamoja.

Walisema kuwa katika hali ngumu ya sasa kutokana na janga la Covid-19, kampuni ya Del Monte haijafuta watu kazi wala kuwapunguzia mishahara hivyo basi kujipa nembo ya “akufaaye kwa dhiki ni rafiki.”

Wabunge hao walisema kuwa Kenya iko na jukumu la kulinda makampuni ya kigeni ambayo yamedhihirisha kuwa na uwezo wa kuinua hali ya maisha ya Wakenya ambao hasa hawana taaluma za kuwapa guu mbele katika soko la ajira.

Walisema kuwa usoroveya huo ukitekelezwa, kunafaa kuzinduliwe mradi mwingine wa kuwafaa wenyeji na ajira ikizingatiwa kuwa vijana wengi kwa sasa wanalia kuwa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta iliwasahau katika kuwabunia mianya ya kujipa riziki.

Siasa za kurefushwa kwa mkataba wa umiliki wa shamba hilo la Del Monte zilianza mwaka wa 2012 wakati Katiba Mpya ilipendekeza wote walio na mikataba ya kipindi kirefu wapigwe msasa tena na maamuzi mapya yaafikiwe kuhusu mikataba hiyo.

Katibu maalum katika wizara ya Mashamba Dkt Nicholus Muraguri aliambia Taifa Leo kuwa serikali haina shida yoyote na mkataba wake na Del Monte.

“Kitu cha kwanza cha kuelewa ni kuwa nakuhakikishia tuitaipa kampuni hii mkataba mpya kwa kuwa imetudhihirishia kwamba iko na uwezo wa kutufaa kiuchumi,” akasema.

Alisema kuwa kesi mahakamani zimekuwa zikikwamiza harakati za k